ByNA GEORGE ODIWUORMAAFISA wa Idara ya Huduma ya Wanyamapori (KWS) Ijumaa wamefaulu kumuua mamba aliyemla mtoto wa miaka 11 katika kijiji cha Manyuru, kaunti ndogo ya Ndhiwa. Katika kisa hicho, mtoto huyo, Felix Odongo wa Gredi ya Pili alikuwa anachota maji na wenzake Mto Kuja wakati alipovamiwa na mamba huyo. “Nilijawa na mshtuko usioelezeka nilipoona mamba huyo akiyoyomea majini na mwanangu,” alihadithia akiwa na majonzi mengi. Wakazi walifurika kumwona mamba huyo alipotolewa mtoni na huzuni ilijaa zaidi pale alipokatwa tumboni mwili wa mtoto huyo ukapatikana. Chifu wa Lokesheni ya Kabuoch Magharibi Ann Anyango alisema mtu mwingine alikufa eneo hilo mwaka jana baada ya kushambuliwa na mamba huyo huyo, jambo linaloashiria hatari kubwa inayokabili wakazi wa eneo hilo.
Source: Daily Nation February 03, 2024 13:13 UTC